''Nina wazo.'' Akainama kwa mbele kama rafiki yangu April afanyavyo anapotaka kusema siri, japokuwa hakuna siri yake iliyo nzuri. Au hata kuwa siri kweli. ''Usipomwambia yeyote kuwa nipo hapa, naweza kuyatibu macho yako''.
''Ondoka mjini!''
Akapepesa mara kadhaa. ''Hicho ndicho ninachojaribu kufanya''.
''Ninachomaanisha ni kuwa huwezi kufanya hivyo!''
''Kwa nini?''
''Kiukweli hakuna mtu ambaye ameweza kuyatibu macho yangu, isipokuwa kwa miwani.''
''Nina uwezo fulani, utaona, kwa kuwa....''
''......Nisimwambie mtu kuhusu wewe?''
''Hilo ni jambo muhimu sana, ndicho kiini.''
''Nitajuaje kuwa hutonipofusha? Unaweza kuwa kama wale wauzaji wa mtandaoni wanavyotoa ahadi lakini ni waongo kabisa.''
Alianza kusafisha, na kusafishwa tena. ''Nisingeweza kufanya jambo lile kwa kiumbe ambacho hakijaniletea madhara yoyote.''
''Unamaanisha kama ningekudhuru, ungenifanya kuwa kipofu?''
''Hiyo ni kwa misingi ya kutaka kujua.''
''Na kama ukiyatibu macho yangu, na nisimwambie yeyote kuhusu wewe,
utaondoka kwenye mashamba yetu?''
''Huo ndiyo msingi wake!''